The House of Favourite Newspapers

Ray C Aibuka Na Mahaba Kimbunga Kutoka Tornado

MWANAMUZIKI maarufu nchini Tanzania Rehema Chalamila ‘Ray C’, baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye ameibuka upya na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la  TORNADO  jina lenye maana ya kimbunga cha mahaba.

 

Ray C anaibuka katika wimbo huo akiwa ameshirikishwa na msanii  kutoka nchini Kenya Dennis Mwangi aka Papa Dennis mwenye makazi yake  nchini Kenya ambapo yupo  chini ya  labo ya Maliza, wimbo huo tayari upo katika video ambayo imetengenezwa nchini Afrika ya Kusini na muongazaji wa video maarufu Afrika, God Father.

 

Mbali na wimbo huo Papa Dennis ameshafanya nyimbo na vinara wengi wa muziki wa Afrika akiwemo Mr Flavour (Nigeria) ,Chiddimna  (Nigeria) ,Korode bello (Nigeria) na sasa Ray – C (Tanzania)

Comments are closed.