The House of Favourite Newspapers

Yanga Bila Mkongo, Chirwa Yaivaa Mwadui FC

KIKOSI cha Yanga jana alfajiri walipanda basi na kuanza safari ya kuelekea mkoani Shinyanga kuwafuata wapinzani wao Mwadui FC bila ya ya nyota wao nane akiwemo Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu na Kocha Mkongo Zahera Mwinyi.

 

Yanga inavaana na Mwadui kesho Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage huko Shinyanga.

 

Chirwa na Ajibu hivi karibuni walitajwa kuwepo kwenye mgomo wa kuichezea timu hiyo katika mechi zilizopita za ligi na Kombe la Shirikisho Afrika kwa kile kilichotajwa kudai mishahara ya miezi mitatu.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, meneja mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema katika msafara huo wachezaji nane pekee ndiyo wamewabakiza kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo majeraha.

 

Saleh aliwataja wachezaji hao kuwa ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Juma Abdul, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Pius Buswita, Chirwa, Donald Ngoma Amissi

Comments are closed.