The House of Favourite Newspapers

Nikki wa Pili Awachana Mastaa Wanaojipoteza Kisa Ujana

Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’

MWANAMUZIKI anayekimbiza na ngoma ya Mawindo, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ amefunguka kwamba kuna mastaa wengi na vijana mbalimbali ambao hufanya mambo ya kuwaharibia maisha yao na kusingizia suala zima la umri kwamba ndiyo tatizo.

Akichonga na Mikito Nusunusu, Nikki alisema kwamba, suala hilo si kweli na umri hauhusiani kabisa kumfanya mtu apoteze ‘future’ yake, bali hujisahau na baadaye mambo yanapowaharibikia hutafuta visingizio.

Nikki alianza kwa kuandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba; ‘Tusizingue kwa kisingizio eti ni ujana umetuchanganya, umri bado sio kisingizio tosha, kuna watoto watiifu na watoto pasua kichwa, kuna vijana wema na wanaojipindisha, kuna watu wazima wa maana na wasio na maana, kuna wazee wana busara na wazee miyeyusho……tusisingizie umri hata mtoto wa darasa la pili anajua usumbufu darasani hautakiwi…..chagua kuwa mtu wa maana, utavuna ya maana!’

 

Alipoulizwa kuzungumzia zaidi kauli yake hiyo Nikki alisema, kila mtu huchagua maisha anayopenda aishi wala umri hauwezi kuwa kigezo.

Stori: Boniphace Ngumije

Comments are closed.