The House of Favourite Newspapers

Kiungo Yanga Kumfuata Samatta Ubelgiji

Emmanuel Martin

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Martin huenda akaachana na timu hiyo na kutimkia Klabu ya Waasland Beveren inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji.

 

Kiungo huyo alijiunga na Yanga kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara akitokea Klabu ya JKU inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Martin alisema kama mipango na taratibu zitakwenda vizuri, basi msimu ujao hatakuwa na Yanga baada ya kuhitajika na klabu hiyo ya Ubelgiji.

 

“Ni kweli hizo taarifa ulizozipata kuwepo na mazungumzo na klabu ya Beveren inayoshiriki ligi nchini Ubelgiji.

“Wiki mbili zilizopita nilipokea simu kutoka kwa mmoja wa mawakala wa nchini Ubelgiji ambaye yeye alipata namba yangu kutoka kwa mmoja wa waandishi wa nchini Rwanda.

 

“Baada ya kupata namba yangu wakala huyo akanipigia simu na kunipa taarifa hizo ambazo nimezipokea na hivi sasa ninavyoongea na wewe nakamilisha baadhi ya vitu ambavyo ameniagiza na baada ya kukamilisha kaniambia nimpe taarifa,” alisema Martin.

 

Kama Martin atafanikiwa kukamirisha mipango hiyo ya usajili, basi atakuwa mchezaji wa pili kucheza soka Ubelgiji baada ya Mbwana Samatta anayekipiga Genk.

Na Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Comments are closed.