The House of Favourite Newspapers

Luke Shaw Anakula ‘Bata La Kufa Mtu’

Beki wa kushoto wa Manchester United, Luke Shaw

BEKI wa kushoto wa Manchester United, Luke Shaw ameweka shida chini na kuamua ku­rusha mikono juu kisha ‘ku­banjuka tu’.

 

Shaw ambaye alikuwa katika wakati mgumu msimu uliopita chini ya Kocha Jose Mour­inho kutokana na kukosa namba kikosi cha kwanza ameonekana kuwa mbali na maisha ya soka baada ya kutumia muda mwingi akila raha.

 

Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye pia ametoswa kwenye timu ya taifa ya Eng­land, ameonekana akiwa kwenye boti bin­afsi akila raha na rafiki zake huku wa­d a d a wakiwa wengi wakim­zungua.

 

Msimu uliopita ali­cheza mechi 11 za Pre­mier League baada ya kuwa chaguo la pili nyuma ya mkong­we Ashley Young.

Comments are closed.