The House of Favourite Newspapers

Cavaliers Yasajili Jembe Nafasi Ya LeBron James

Channing Frye.

CLEVELAND Cavaliers imeendelea kuimarisha kikosi chake baada ya kumnasa mkongwe Channing Frye.

Timu hiyo inafanya usajili wa nguvu ili kuhakikisha inajiweka vizuri baada ya kuondokewa na staa wake, LeBron James.

 

Frye amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Dola milioni 2.4 ili kuchezea Cleveland Cavaliers kwenye msimu ujao wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA).

 

Staa huyo, hata hivyo sio mgeni kwenye kikosi cha Cavaliers kwani alikuwemo katika kikosi kilichotwaa ubingwa mwaka 2016.

 

Frye, ambaye ni mkongwe wa mpira wa kikapu, ataisaidia Cavaliers likija suala zima la uzoefu.

 

Staa huyo ana uzoefu mkubwa na mpira wa kikapu kutokana na kucheza misimu 13 ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA).

Comments are closed.