The House of Favourite Newspapers

Nandy ‘Achojoa’ Nguo Kiatu Jukwaani!

KUONESHA mzuka umemkolea, msanii wa Kizazi Kipya zao kutoka Jumba la Kuibua Vipaji Tanzania (THT), Faustina Charles ‘Nandy’ amejikuta akishindwa kuzuia hisia zake mbele ya mashabiki na kulazimika kuvua ‘kuchojoa’ nguo ya juu pamoja na kiatu kimoja.

 

Ishu nzima ilijiri pande za Nyamongo, Tarime ambapo msanii huyo alikuwa akitumbuiza na baada ya kufika katikati ya shoo alisikika akiwaambia mashabiki wake kwamba avue nguo asivue ndipo akavua na kuwarushia akibakiwa na nguo moja ya ndani.

 

Baada ya muda tena aliwarushia kiatu mashabiki na kufanya umati uendelee kulipukwa kwa shangwe. Hata hivyo mara baada ya kushuka kwa shoo hiyo, Nandy aliingia katika mtandao wake wa Instagram na kuwashukuru mashabiki hao kwa kuandika; “Juhudi huzidi kipaji, asanteni sana Nyamongo

Comments are closed.