The House of Favourite Newspapers

NMB na Halotel washirikiana kutoa kompyuta, intaneti kwa shule 200 za Serikali

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (Mbele kulia), akisaini mkataba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Nguyen Van Son, utakaowezesha shule zaidi ya 200 za serikali kupata kompyuta na inteneti bure, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko Halotel, Mhina Semwenda na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd.

Benki ya NMB kwa kushirikiana na Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel zimeingia katika makubaliano yatakayo wezesha shule zaidi ya 200 za serikali kupata kompyuta na Intaneti bure. Ushiriakiano huu una lengo la kuboresha mfumo wa kujifunza na ufundishaji kupitia teknolojia katika shule za Msingi na Sekondari nchini.

 

 

Katika ushirikiano huo utakao dumu kwa miaka miwili benki ya NMB itatoa zaidi ya kompyuta 350 kwa shule 100 huku zikiunganishwa na huduma ya intaneti kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel. Hii ni huduma endelevu ambapo kwa miaka minne (4) iliyopita zaidi ya Kompyuta 600 zilitolewa kwa shule mbalimbali ambazo Halotel itaunganisha intaneti katika shule hizo za awali na kwa mwaka huu wa fedha kuna zaidi ya kompyuta 400 zitakazotolewa kwa shule zaidi ambazo zitaunganishwa moja kwa moja na huduma ya Intaneti.

 

 

Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker amesema benki hiyo imejidhatiti katika kutumia sehemu ya faida inayopatikana ili kuisaidia jamii.

 

 

“Kwa miaka mingi, NMB kupitia mipango ya Majukumu, wajibu wa kampuni katika Jamii ( CSR ) imewekeza na kuzingatia upatikanaji wa elimu kwa serikali za mitaa kwa kuchangia madawati ya shule, ujenzi wa vyumba vya kujisomea na pia kutoa kompyuta kwa ajili ya kujifunza na kufundisha kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ushirikiano huu unadhihirisha kwamba tunasonga mbele kupitia teknolojia “.

 

 

“Katika Ushirikiano huu mahsusi na Halotel, tutatoa kompyuta kwenye shule za Serikali zaidi na Halotel wataziunganisha na huduma ya intanenti. Tumekubaliana pia shule ambazo Halotel tayari inatoa huduma ya intaneti na sisi tutatoa kompyuta. “Alisema Bi Bussemaker.

 

 

“Kwa mwaka 2018/2019 tayari tuna kompyuta 350 za kutoa, tunaamini zitaleta mchango mkubwa katika kujifunza Teknolojia ya Mawasiliano na Habari katika shule na baadaye kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia” alifafanua zaidi Ms. Bussemaker.

 

 

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Nguyen Van Son, amesema, hii si mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kuunga mkono sekta ya elimu nchini. Kampuni hiyo imesaidia mipango kadhaa kuelekea maendeleo ya sekta ya elimu nchini Tanzania na tayari imeshatoa vifaa mbalimbali vya elimu kama vile madawati ya shule, vitabu, mabegi , kujenga madarasa na kuweka vifaa vya kufundishia na kujenga miundombinu na kuungaisha bure huduma ya intaneti kwa Shule zaidi ya 417 nchini kote.

 

 

Tofauti na mipango mingine kama hiyo, Halotel kwa ushirikiano na kitivo cha CoICT  cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imeanzisha jukwaa la kujifunza linayoitwa Halostudy (http://www.halostudy.ac.tz/) lenye maudhui ya Sayansi na Hisabati kwa masomo yote kuanzia Kidato cha Kwanza mpaka cha nne inayofuata mtaala wa shule za sekondari za Tanzania. Maudhui yaliyotengenezwa yameunganishwa na vipengele vya njia mbalimbali za mawasiliano  kama vile video, sauti, sauti na michoro katika maeneo maalum ambapo ni shida kuelewa maudhui kutumia maandishi pekee.

 

 

“Tuna hakika kwamba ushirikiano huu utaongeza hamasa katika kutumia jukwaa la kujifunza la Halostudy kuruhusu wanafunzi na walimu kuweza kutumia jukwaa hili kwa utendaji mzuri katika masomo yao na hivyo kuleta matokeo chanya katika sekta ya elimu. Halotel itaendelea kuwekeza zaidi kuwezesha shule za serikali kuunganishwa na huduma ya intanenti ili kuboresha Mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kufundisha na kujifunza “. Alisema Son.

 

 

“Ushirikiano huu unadhihirisha wazi umoja baina ya kampuni zinazoungana na kushiriki katika kusaidia sekta ya elimu ya nchini kwa kuweka Mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano utakaosaidia katika kufundisha na kujifunza katika shule za serikali.” Aliongeza, Son.

 

 

Muingiliano wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwenye elimu katika wazo la kufundisha-kujifunza daima hufundisha teknolojia. Sio tu kuhusu kutumia teknolojia na kuwa mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano lakini pia kufanya mchakato wa kujifunza zaidi kuvutia,kuleta furaha na kushiriki kwa pamoja kati ya walimu wote na wanafunzi. Ushirikiano huu utawasaidia wanafunzi kukuza uanzishwaji, ubunifu, na kufikiri muhimu.

 

 

Comments are closed.