The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu Amwaga Matusi Mbele Ya Mashehe

Lulu Eugene ‘Amber Lulu’.

Ustaarabu una watu wake lakini si kwa msanii wa kizazi kipya Lulu Eugene ‘Amber Lulu’ ambaye Jumapili iliyopita alimwaga matusi mazito mbele ya mashehe waliokuwa wakisafiri kwa ndege kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam, Amani lilishuhudia laivu tukio hilo.

 

Idadi ya mashehe waliosikia ‘domo’ la msanii huyo likimwaga mitusi ni saba, kibaya zaidi miongoni mwao alikuwepo Mufti wa Tanzania Abubakary Zuberi na Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, mashehe wanaoheshimika.

 

TUKIO LILIKUWAJE?

Amber Lulu na wasanii wenzake akiwemo Farid Kubanda ‘Fid Q’, Juma Mohammed Mchopanga ‘Jay Mo’ na Meseni Selekta

walikuwa Mwanza kwenye shoo na kwamba walitumia usafiri wa ndege kuwarudisha Dar ambapo wakati wa safari walikutana ndani ya ndege na mashehe hao ambao nao walikuwa safarini kuelekea Dar.

Kama ulivyo utaratibu, kila msafiri aliketi kwenye kiti chake sehemu tofautitofauti lakini Amber Lulu alikuwa kiti cha nne nyuma ya Mufti upande ambao mashehe wengine pia walikuwa wamekaa.

 

Haikujulikana kama ni ulevi au ndiyo akili za msanii huyo imepinda; alianza kufanya mambo ambayo hayakuwa

ya utulivu jambo ambalo lilifanya msafiri mwingine aliyekuwa amekaa karibu ashauri msanii huyo ahamishiwe siti ya nyuma.

 

Kwa nini? Busara ilimuongoza msafiri huyo kuwa, jinsi msanii huyo alivyokuwa na vituko vya hovyo isingependeza avifanye mbele ya mashehe na kwamba kumrudisha nyuma kungeepusha mambo ya kuharibiana ustaarabu.

 

AMBER LULU AANZA KUFYATUA MATUSI

Baada ya kutoa ushauri huo ambao sauti yake ilisikiwa na Amber Lulu, mashetani ya msanii huyo yakaamka na swali la kwanza likawa “Kwa nini nikakae

“Kuna mtu kalipa milioni humu …(tusi zito)” sauti za “astaghfirullah” zikasikika kuashiria kuna watu walikuwa wakiomba msamaha kwa Mungu.

 

Kuashiria kwamba aliyekuwa akiombewa msamaha zaidi hajitambui akaporomosha tusi tena, kisha akanyanyuka kama mtu anayesema “mtanifanya nini?” Akaaga kwa sauti:

“Naenda chooni nilikirudi huko nataka kumjua aliyeniambia nihamie nyuma… (tusi zito tena) sauti za “astaghfirullah” zikafuatia.

 

AMBER LULU ATOKA CHOONI

Matarajio ya wengi yalikuwa ni kumuona Amber Lulu akitimiza ahadi yake baada ya kutoka chooni ya kumsaka mbaya wake lakini aliporejea alikuwa na aibu nyingine nzito zaidi.

Hapa tena sauti za kuomba toba kwa Mungu hazikusikika  lakini wasafiri wengi wakiwemo mashehe waliinamisha vichwa kuzuia macho yao yasione nyeti za Amber Lulu.

 

 

Imekuwaje tena? Kwamba alipokwenda maliwatoni msanii huyo alisahau kujistiri vizuri na kujikuta akitoka huko ‘chakula ya mtoto’ iko nje na baadhi ya sehemu nyeti za mwili zikionekana.

 

MHUDUMU WA NDEGE AINGILIA KATI

Kufuatia vituko vya msanii huyo kuzidi mhudumu wa ndege alitangaza kwenye kipaza sauti: “Kama kuna msafiri hataki safiri bora ashuke.”

Hapo ndipo Amber Lulu alipotii na kuketi kisha ndege ikapaa majira ya saa 3:45, usiku na kufika Dar saa 4:25 ambapo wauliza maswali “Huyu nani?” walikuwa wameshaambiwa “Ni Amber Lulu msanii wa muziki wa kizazi kipya.”

Vilio,Majonzi! Vyatawala Mazishi ya Mama wa Shigongo

Comments are closed.