The House of Favourite Newspapers

KESI YA AVEVA: MAHAKAMA YATAKA HATI YA MASHITAKA IKAMILISHWE

Evans Aveva na Godfrey Nyange ‘Kaburu’ walipofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo.

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  imetoa siku saba kwa upande wa mashtaka kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka katika kesi inayomkabili Evans Aveva na Godfrey Nyange ‘Kaburu’.

 

 

Agizo hilo limetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba, baada ya Mwendesha Mashtaka wa  Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru)  Leonard Swai kueleza kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kutajwa.

 

 

Agizo la kubadilishwa kwa hati ya mashtaka inatokana na amri iliyotolewa Agosti 10, mwaka huu kwamba upande wa mashtaka umuondoe Zacharia Hans Poppe na Frank Lauwo ili kesi  iweze kuendelea.

 

 

Kwa uande wake,  mshtakiwa Aveva aliiomba mahakama  wapewe muda wa siku saba kwa sababu siku 14 ni nyingi na upande wa mashtaka umekuwa ukichelewesha jambo hilo na wao wanaumia kukaa mahabusu.

 

Baada ya hapo, Hakimu Simba amesema anatoa siku saba kwa upande wa mashtaka kukamilisha taratibu za kubadilisha hati ya mashtaka ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 17, mwaka huu.

 

 

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka kumi yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi,  kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha.

 

Comments are closed.