The House of Favourite Newspapers

Duh! Yanga Wameanza Mikwara

MWINYI Zahera yuko DR Congo akiifundisha timu ya Taifa ya nchi hiyo lakini amewaambia Simba wajiandae kwavile Yanga sasa ipo tayari kwa mapambano.

 

Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa DR Congo hatokuwa kwenye kikosi cha Yanga kitaka­chocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Singida United Septemba 5, mwaka huu mkoani Kigoma kutokana na kuwa na majukumu mengine.

 

Ameliambia Championi Jumamosi kuwa, haoni tabu tena kwenye kikosi chake kama ilivyokuwa huko nyuma am­bapo wachezaji wengi walikuwa na migomo ya hapa na pale, lakini sasa suala hilo limekwisha kilichobaki ni kazikazi hivyo timui pinzani zijiandae ikiwemo Simba.

“Nina kikosi kizuri sana hasa ukiangalia umri wa wache­zaji wangu bado ni bora zaidi ya wengine jambo linalonipa moyo kuwa tutafanya vizuri sana kwenye ligi maana kikosi changu ni kipana na kinato­sha kabisa kugawika hata kwa uwiano wa michezo sawa ya ligi,”alisema Kocha huyo ambaye anaishi karibu na ufukwe wa Bahari ya Hindi upande wa Kawe.

 

“Hadi sasa nina safu bora ya ush­ambuliaji tofauti na wengi kuendelea kumta­zama Makambo (Heritier) pekee wakati nina watu wazuri kama Matheo (Anthony), Mhilu (Yusuf), Nkomola (Yohana) na wengine wengi kama kina Kaseke na Mrisho Ngassa na hawa wote wanaumri mzuri unaoweza kurekebisha na kuja kufanya maajabu nje ya matarajio ya wengi.

 

“Kuna watu wengi wame­kuwa wakidhania kuwa Simba tu ndio ina mtaji wa mastraika huku wakiibeza Yanga jambo ambalo si kweli kama tuna kikosi ki­bovu kiasi hicho na ukitaka kufahamu kuwa Yanga ina vikosi zaidi ya viwili basi ni nafasi ya kila mmoja kusubiria mbio za ligi zizidi kusonga na baadaye wataona ninachokimaanisha,” alisema Zahera.

Musa Mateja,Dar es Salaam

Comments are closed.