The House of Favourite Newspapers

WOLPER: Harmonize Bado Ananipenda, ni Pepo Tu – Video

MSANII wa filamu nchini na mjasiriamali, Jacquiline Wolper amesema katika historia yake ya mahusiano kila mwanamume anayeachana naye anakuwa bado anamuhitaji licha ya yeye kuwakacha na kutohitaji mawasiliano nao wala kusogeleana.

 

Woler amesema hayo usiku wa kuamkia leo  kwenye ukumbi wa King Solomoni wakati akihojiwa na wanahabari kuhusu kukataa kukimbia salam ya Harmonize hivi karibuni kwenye moja ya event.

 

“Ujue mimi kila nikiachana na mwanaume anakuwa bado ananipenda, pale nilikimbia kwa sababu nikiachana na boyfriend, huwa sipendi niendelee kuwasiliana naye wala kusogeleana naye, sipendi kusalimiana na X.

 

“Ilishawahi kutokea X ananihitaji kwa ajili ya mambo ya kibiashara lakini kwa sababu nakuwa sihitaji kabisa kuwasiliana nao nili-crash halafu nikakosa dili, hilo ni pepo ambalo ninalo nadhani nitamwambia mchungaji aniombee,” alisema Wolper.

 

Akizungumzia sakata la kukacha ujaji wa Miss Lake Zone, Wolper amesema taji hilo limeshapoteza mvuto ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hivyo walitumia jina lake ili kuwavuta watu japo ilibuma.

 

VIDEO: MSIKIE HAPA WOLPER AKIFUNGUKA

Comments are closed.