The House of Favourite Newspapers

Mazoezi Ya Simba Usipime, Yawekewa Ulinzi

BAADA ya Simba kubaki jijini Dar na kuweka kambi katika Hoteli ya Sea Scape iliyopo Mbezi Beach, jana Jumatano kikosi hicho kilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko.

 

Katika mazoezi hayo, uongozi wa Simba uliwawekea ulinzi mkali nyota wake hao kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Katika mazoezi hayo ya jana, licha ya mashabiki kuwepo hapo uwanjani lakini kulikuwa na makomandoo kadhaa ambao walikuwa wanazungu kazunguka wakati mazoezi yakiendelea.

 

Hata hivyo, katika mazoezi hayo, wachezaji wa Simba walionekana kufanyishwa mazoezi ya nguvu na makocha wa kikosi hicho.

Katika zoezi hilo, wachezaji walionekana wakipambana licha ya baadhi yao kulalamika kutokana na aina ya mazoezi ambayo walikuwa wanayafanya kuonekana ni ya nguvu.

Katika mazoezi hayo, Hassan Dilunga na Mzamiru Yassin ndiyo wachezaji ambao hawakufanya mazoezi na wenzao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ni majeruhi.

Katika mazoezi hayo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Masoud Djuma alionekana uwanjani akiendelea na majukumu yake kama kawaida licha ya kwamba hapo awali hakusafiri na timu ilipokwenda kucheza mikoani ikiripotiwa kutokuwa na maelewano mazuri na wenzake wa benchi la ufundi.

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

Comments are closed.