The House of Favourite Newspapers

Mourinho Ana Saa 24 Man United

Kocha Jose Mourinho.

MUDA wa Kocha Jose Mourinho kuendelea kuwepo ndani ya Man­chester United umebaki mfupi na hiyo inatokana na Mreno huyo kuendelea kutibuana na wachezaji wake na sasa mbaya zaidi ni kuwa hata mabosi wake wanaelekea kufikia ukomo wa uvumilivu.

 

Taarifa kutoka klabuni hapo zi­naeleza kuwa ikiwa Man United itapote­za mchezo wa kes­ho Jumamosi dhidi ya Newcastle kati­ka Premier League basi kibarua chake kitakuwa kimeota nyasi.

 

Habari hizo zimepewa n g u v u z a i d i h a s a k w a k u w a k o c h a wa za­m a n i w a R e a l M a ­d r i d , Z i n ­edine Z i ­dane n a y e inaelezwa kuwa yupo tayari kube­ba mikoba baada ya Mreno huyo ku­fukuzwa.

 

Bodi ya United ilikuwa tayari ku­muunga mkono kwa kuwa ndani ya misimu miwili ali­yodumu kulikuwa na maendeleo uwanjani tofauti na wenzake wawili waliomtangulia la­kini kwa mwelekeo wa timu ulivyo sasa hali inaweza kuwa tofauti.

Siku tatu zilizopi­ta nguli wa United, Paul Scholes alisema anashangaa kuona ko­cha huyo hajafukuzwa mara baada ya timu kufungwa mabao 3-1 dhidi ya West Ham.

 

United imeanza msimu vibaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1989, ikiwa im­eshatolewa katika Carabao Cup, inazidiwa pointi tisa na vinara wa Premier na ilishindwa kui­funga Valencia, Jumanne iliyo­pita katika Ligi ya Mabingwa.

 

Roy Keane amtetea Mour­inho

Nahodha wa zamani wa United, Roy Keane amemuunga mkono Mourinho na kusema kuwa kuna ‘watoto wengi wana­lialia’ katika soka la sasa.

“Siyo kila mchezaji atapatana na kocha, lakini unachotakiwa kukifanya ukiwa mchezaji ni kutimiza waji­bu wako, niliwahi kukwaruzana na makocha kadhaa lakini bado nilicheza kwa faida ya timu.

 

“Sijali umekwaruzana vipi na kocha au mtu mwingine, un­apokuwa Man United utambue ni moja ya klabu kubwa duniani na kuna vitu vitakuzwa, unapo­vaa jezi ya United unatakiwa kupambana kwa asilimia 100.

 

“Mchezaji anayegombana na kocha kisha anacheza chini ya kiwango siyo mchezaji, siku hizi kuna watoto wengi wanalialia, namtakia kila la kheri Mourin­ho kudili na kazi yake,” alisema Keane.

Comments are closed.