The House of Favourite Newspapers

Okwi Aanza Kutupia Taifa, Masoud Djuma Baibai Simba

African Lyon

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara wamerudi mchezoni. Mabao ya mastraika Shiza Kichuya na Emmanuel Okwi, jana usiku yalitosha kuwapa Simba ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa.

Simba ambayo ilikuwa bila kocha wao msaidizi, Masoud Djuma ambaye inadaiwa amepigwa chini, ilimiliki sehemu kubwa ya mchezo huo huku ikikosa mabao mengi ya wazi.

Kikosi cha Simba.

Kichuya alipachika bao lake dakika ya tisa akiunganisha vizuri pande la kiraka aliyewahi kufanya majaribio Ufaransa, Shomari Kapombe.

Okwi alimaliza mchezo mwanzoni mwa kipindi cha pili kwa bao lake la kichwa akimalizia krosi ya beki Mohammed Hussein katika dakika ya 48 ya mchezo huo.

 

Bao pekee la Lyon lilifungwa na Awadhi Juma dakika 61 kwa shuti kali la nje ya boksi huku Haruna Niyonzima akiingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Claytous Chama.

Mastraika wa Simba walikosa nafasi nyingi za wazi kutokana na papara walipokuwa wakifi ka kwenye eneo la hatari, huku mabeki wa Lyon wakionyesha ukomavu wa aina yake na kutokuwa na papara.

 

Kocha wa Simba, Patrick Aussems, alikerwa na kitendo cha kutengeneza nafasi nyingi na kushindwa kupachika mabao ya kutosha lakini akasema lengo ilikuwa ni ushindi wa mapema sana kama alivyofanya Kichuya.

MASOUD BAIBAI

Uongozi wa Simba umefanya maamuzi magumu baada ya kumng’oa kwenye benchi kocha kipenzi cha mashabiki, Masoud Djuma.

Kocha kipenzi cha mashabiki, Masoud Djuma.

Masoud hakuwepo kwenye benchi la Simba jana usiku katika mechi dhidi ya African Lyon na licha ya kwamba viongozi wamekuwa wagumu kufafanua lakini Spoti Xtra limejiridhisha kwamba biashara ya Masoud na Simba imekwisha.

Habari zinasema kwamba Masoud alikutana na muwe- kezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ juzi Ijumaa jioni na kufi kia maku-baliano ya kuvunja mkataba baada ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems kuweka wazi kwamba hayuko tayari kufanya naye kazi.

 

Habari zinasema kwamba Aussems amewaambia viongozi kuwa Masoud ana mambo ambayo hayawezi kuipa timu mafanikio, hivyo hawezi kuendelea kukaa naye ndani ya timu kwa madai kuwa atamvuruga.

 

Mmoja wa vigogo wa Simba aliyefanikisha ujio wa Masoud nchini ambaye amewahi kushikilia nafasi ya juu kwenye uongozi wa TFF enzi hizo akiwa mtumishi wa umma, juzi jioni alikwenda kambini kumshawishi Aussems lakini akamwambia ; “Hapana Masoud simtaki.”

Spoti Xtra limejiridhisha kuwa Masoud jana alibeba kila kilicho chake kwenye kambi ya Simba iliyoko katika Hoteli ya Seascape na ameaga wachezaji na kuwatakia kila la kheri. Masoud anatarajiwa kuondoka nchini leo au kesho kwa usafi ri wa barabara akitumia gari yake binafsi kurejea kwao Burundi.

Matokeo mengine ya jana

Singida 3-1 Ndanda

Prisons 1-2 Mbeya City

Kagera 0-0 Ruvu

Shooting Mtibwa 1-1 KMC

STORI: SAID ALLY NA IBRAHIM MUSSA ,  PICHA NA MUSA MATEJA

MAGAZETI OCT 07: Saluti yamhenyesha Ofisa Magereza mbele ya Waziri

Comments are closed.