The House of Favourite Newspapers

RAIA WAWILI WA CHINA WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA  MIAKA 2

Raia wa wawili wa china na mtanzania mmoja wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kufikishwa leo.

 

 

Raia wa wawili wa china na mtanzania mmoja  leo wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ama kulipa faini ya Milioni 9.3 wafanyakazi wa Kampuni ya Jiangxi Internatiol (T) Investment Ltd baada ya kukiri makosa ya kushindwa kuchukua tathmini ya uharibifu wa mazingira.

 

 

Washtakiwa hao ni Injinia Xia Yanan (26), Chen Jinchuan (31) na Mtala Habibu (29) fundi umeme. Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali Nassoro Katuga kuwasomea washtakiwa makosa yao na kukiri.

 

 

Hakimu Shaidi amesema kutokana na washtakiwa kukiri makosa yao mahaka inawahukumu kulipa faini ya Shilingi Milioni Tisa na laki Tatu ama kwenda jela miaka miwili.

 

 

Hakimu Shaidi amesema katika kosa la kwanza la kushindwa kuchukua tathmini ya uharibifu wa mazingira,wanatakiwa kulipa Shilingi Milioni tatu kwa kila mshtakiwa ama kwenda jela miaka miwili.

 

 

Pia kosa la pili la kutotii amri halali ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), watuhumiwa hao walitakiwa kulipa faini ya Shilingi laki moja ama kwenda jela miaka miwili.

 

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari na Agosti 28,2018 maeneo ya Regent Estate Kinondoni na kosa la kutotii amri ya (NEMC) ya kusimamisha ujenzi, walilitenda Agosti 25,mwaka huu ambapo katika hati ya mashtaka inaeleza kuwa waliendeleza ujenzi bila kuchukua tahadhari ya mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

 

 

Washtakiwa hao wamefanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kuachiwa huru.

Comments are closed.