The House of Favourite Newspapers

Mashabiki Wamvamia Masau Bwire Mwanza

 

Masau Bwire

OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, juzi Jumatano alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na mashabiki na kuanza kumzomea baada ya timu yake kuchapwa mabao 3-0 na Alliance Schools.

 

Bwire alikutana na tukio hilo kabla ya mapumziko katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini hapa. Championi Ijumaa ambalo lilikuwepo uwanjani hapo, liliwashuhudia mashabiki wa Alliance Schools wakimzonga

 

Bwire ambaye alikuwa amekaa kwenye gari la timu yao. Mara baada ya mchezo huo kumalizika, Bwire aliliambia Championi Ijumaa kuwa, aliamua kukaa kwenye gari hilo ili mashabiki wasimuone, lakini alijikuta tayari ameonekana na kumvamia.

STORI NA Johnson James

Comments are closed.