The House of Favourite Newspapers

Zahera Ataja Nondo 3 Simba iimalize As Vita

Mwinyi Zahera

KOCHA Msaidizi wa timu ya Taifa ya DR Congo na Klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ameipa Simba mbinu ya ushindi leo itakapokuwa ikivaana na AS Vita ya Congo. Timu hizo zinavaana leo kwenye Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte uliopo Kinshasa, DRC Congo katika mchezo wa Kundi D ambapo pia kuna timu za Al Ahly na JS Soura.

 

Katika mchezo huo, Simba wataingia uwanjani wakiwa wa morali ya hali ya juu baada ya kupata ushindi katika mchezo wake wa awali wa mabao 3-0 dhidi ya JS huku AS Vita wao wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mabao 2-0 na Al Ahly.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Zahera alisema Simba kama wanataka ushindi wa ugenini basi Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Patrick Aussems, anatakiwa aingie uwanjani kwa lengo moja pekee la kupata pointi tatu
na siyo sare.

Zahera aliongeza kuwa kama Simba wakiingia na mbinu hiyo ya ushindi na siyo kujilinda, basi watafanikiwa kurejea nchini na pointi tatu kutokana na uimara wa kikosi cha Simba kinachoundwa na wachezaji wengi wenye uzoefu ambao ni Claytous Chama, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.

 

“Simba ninaipa asilimia 50 ya kushinda mechi yao na AS Vita, kwani mimi ninaifahamu vizuri timu hiyo kwani viwango vya wachezaji wake havitofautiani sana na Simba wote wanalingana. “Kikubwa wanachotakiwa kukifanya Simba ni kuwa, wanatakiwa waingie uwanjani kwa lengo moja pekee la kushambulia ndani ya wakati mmoja wanajilinda kutokana na ugumu wa mchezo huo.

“Simba hawatakiwi kukaa golini kwao kwani kutawapa nafasi wachezaji wa AS Vita kusogea golini kwao na kwenda kuwashambulia, lakini wakicheza kama walivyocheza na wale Algeria (Saoura) hapa nyumbani, basi ninakuhakikishia watarejea nyumbani na pointi tatu,” alisema Zahera ambaye bosi wake timu ya taifa Florent Ibengé ndiye kocha wa Vita

Comments are closed.