The House of Favourite Newspapers

OKWI AUNDIWA TUME MAALUM MISRI

Mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi.

WAKATI homa ya mechi ya kimataifa ya mabingwa Afrika kati ya Simba na Al Ahly ikizidi kupamba moto, imebainika kuwa mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi ndiye mchezaji anayewapasua vichwa vilivyo viongozi wa benchi la ufundi la Waarabu hao.

 

Hiyo ni kutokana na rekodi nzuri aliyonayo dhidi ya timu za Waarabu ambapo kila ana­pokutana nao uwanjani mara nyingi amekuwa akiwasumbua.

 

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima ameliambia Championi Iju­maa kuwa mara tu baada ya kufika Misri walipata taarifa kuwa Okwi ndiye anaye­waogope­sha zaidi Waarabu hao na tayari beki wa zamani wa TP Maz­embe ya DR Congo, Mmali, Salif Coulibaly ambaye anawatumikia Waara­bu hao kwa sasa, amepatiwa jukumu la kumdhibiti.

 

“Hiyo ndiyo taarifa mpya ambayo tumeipata hivi kar­ibuni, lakini tunaendelea vizuri na maandalizi yetu na katika mechi hiyo ya Jumamosi tuta­pambana vilivyo kuhakikisha tunafanya vizuri.

 

“Kwetu sisi tunahitaji ush­indi katika mchezo huo na kama siyo ushindi basi sare lakini siyo kupoteza mch­ezo huo, kwa hiyo pamoja na kumwekea ulinzi mkali Okwi lakini bado naamini tutafanya vizuri tu,” alisema Niyonzima.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.