The House of Favourite Newspapers

Nyota Simba wamsapraizi Aussems Misri

Mbelgiji Patrick Aussems

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amefunguka kuwa licha ya kuwa na baridi kali lakini bado wachezaji wake wameonyesha morali ya juu katika kufanya mazoezi kuhakikisha wako tayari kupambana dhidi ya Al Ahly ya Misri.

 

Simba, kesho itakuwa ugenini dhidi ya Al Ahly katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Makundi ambao uta­pigwa kwenye Uwanja wa Borg El Arab.

 

Simba itakuwa ikitupa karata yake ya tatu katika hatua ya makundi baada ya kuivaa, JS Saoura na AS Vita Club na kuwa nafasi ya tatu katika kundi hilo.

Akizungumza kutoka Misri, kocha huyo alisema kama timu wanaendelea vizuri ku­fanya maandalizi yao ya mwisho licha ya kuka­biliwa na hali ya baridi ambayo ni tofauti na ile ya Tanzania.

 

“Japo kuna baridi kali lakini vijana wanaonye­sha ari ya kupambana, wanafanya mazoezi kwa bidii na sisi tumefanya mazoezi usiku hivyo tunaendelea kujiweka sawa na wachezaji wote ambao wamekuja huku wote wako fiti.

 

“Kurejea kwa John Bocco kwenye kikosi nako kumeleta ha­masa kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wache­zaji, ninaamini mpaka kufika Jumamosi kila kitu kitakuwa sawa na lengo ni ushindi kama ni hali ya hewa tutaendelea kupambana nayo,” alisema Mbelgiji.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.