The House of Favourite Newspapers

SIMBA NA YANGA MZIGONI LEO LIGI YA WANAWAKE

LIGI ya wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League inaendelea leo timu 12 zitakuwa mzigoni kutafuta pointi tatu kwenye viwanja vitano.

 

Evergreen Queens watakuwa uwanja wa Karume wakicheza na Siterz FC, Mapinduzi Queens watakuwa uwanja wa Sabasaba wakimenyana na Alliance Girls (Njombe), Panama FC watakuwa Uwanja wa Sabasaba wakimenyana na JKT Queens.

Tanzanite SC itakuwa uwanja wa AmrAbeid ikimenyana na Baobab Queens na Mlandizi Queens watakuwa uwanja wa Mabatini wakimenyana na Yanga Princess na Simba Queens watamenyana na MarshQueens uwanja wa Karume.

 

Mechi zote za leo zitaanza saa 10:00 isipokuwa ile ya Evergreen Queens na Sisterz FC itaanza saa 8:00 uwanja wa Karume.

Comments are closed.