The House of Favourite Newspapers

Yanga Kukipiga na Coastal Mkwakwani Tanga leo

Kikosi cha timu ya Yanga SC.

YANGA leo itakuwa ugenini kucheza na Coastal, lakini rekodi za timu hizo kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga zinaonyesha kwamba kila timu imechukua pointi sawa tangu mwaka 2011/12.

 

Lakini Yanga inayoongoza ligi kwa pointi 53, wanatua kwenye Uwanja huo wakiwa na kiburi kwa madai kwamba hawajawahi kupoteza dhidi ya Coastal mwezi Februari kwani mara ya mwisho walishinda bao 1-0.

 

Coastal ambao wana pointi 28 wakishikilia nafasi ya saba, dhidi ya Yanga wameshinda mara mbili na sare moja huku Yanga takwimu zao zikiwa hivyohivyo. Lakini msimu huu, wanaenda kukutana wakiwa na mabadiliko katika vikosi vyao ambavyo mara ya mwisho walikutana kwenye uwanja huo msimu wa mwaka 2015/16 kabla ya kushuka.

 

Mkongo, Mwinyi Zahera wa Yanga anasema; “Malengo yetu kama kawaida ni kuona tunashinda kila mchezo na hilo nawaeleza wachezaji wangu kila siku hakuna timu ya kudharau.

 

” Kocha wa Coastal, Juma Mgunda anasema “Yanga sio timu ya kudharau wako vizuri na wana kikosi bora hatuwezi kuwadharau lakini sisi tunahitaji kuondoka na ushindi wa pointi tatu.”

 

Kiungo mshambualiji wa Coastal Union , Athuman Idd “ Chuji” amesema kwa tizi waliyopigishwa na makocha wao takribani wiki moja linatosha kuwamaliza Yanga leo.

 

Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga alisema; “Tunaiheshimu Yanga SC kwanza ni timu yenye wachezaji wazuri na wazoefu lakini lazima kitaeleweka tu.”

Comments are closed.