The House of Favourite Newspapers

Yanga Yataja Hujuma Za Ubingwa

Kikosi cha timu ya Yanga SC

KAIMU Mwenyekiti wa Yanga, Samweli Lukumay, amefunguka kuwa wapinzani wao wameanza kuwahujumu kwa lengo la kuwavuruga makusudi kutokana na kusambaza maneno yaliokosa ukweli kufuatia matokeo ya sare mfululizo kwenye Ligi Kuu Bara.

 

Yanga wamekuwa wakihu­sisha hujuma hizo na mchezo wao wa Februari 16 utakao­pigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Simba.

 

Yanga inaongoza ligi kuu ikiwa na pointi 54 ikiwa ikipoteza mchezo mmoja na kutoka sare mbili mfululizo hali iliyosaba­bisha kuwepo kwa taarifa za mgomo baridi wa wachezaji wa timu hiyo uliotokana na vion­gozi wasiomtaka Mwinyi Zahera kufuatia kuingilia suala la fedha za michango ya timu.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Lukumay alisema mpango huo unafanywa na wapinzani wao wakiwemo Simba kwa lengo la kutaka kuwatoa mchezoni kutokana na kuongoza ligi kwa pointi nyingi.

 

“Kwanza nikutoe hofu, Yanga hakuna kitu kama hicho na wala wachezaji au viongozi hawawezi kukaa kujenga mipango hiyo michafu, huo ujumbe hata sisi tunauona ukitembea mitandao­ni lakini siyo kweli.

 

“Unajua hapo ni wapinzani wetu am­bao wao wanatafu­ta kila sababu ya kutuondoa kwenye mipango yetu ila kuhusu sare za mikoani uongozi tunaelewa ugumu wa viwanja vya huko na hizo ni hujuma am­bazo wamezianzisha,” alisema Lukumay.

Comments are closed.