The House of Favourite Newspapers

Julio: Simba SC watashinda kwa mipango

KOCHA wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye alishawahi kuinoa Simba, amefunguka kuwa, kikosi hicho kitashinda mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly ya Misri kutokana na mipango inayofanywa na benchi la ufundi la timu hiyo.

 

Simba walipoteza mchezo wao wa ugenini dhidi ya Al Ahly kwa mabao 5-0, ambapo wanatarajia kurudiana Februari 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kusaka nafasi ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Julio alisema uwezo wa kuwafunga Al Ahly ni mkubwa, kutokana na mipango ambayo benchi la ufundi la Simba inaipanga, huku akiweka wazi kuwa mbinu pekee ya kuwaamaliza Waarabu hao ni mipango itakayofanyika nje na ndani ya uwanja.

 

“Bila mipango wale Waarabu ni ngumu kuwafunga, ila naliamini benchi la Simba lazima litasuka mipango ya ndani na nje ya uwanja ili kuweza kupata pointi mbele ya Waarabu, inawezekana kabisa timu yetu kushinda mchezo huo,” alisema Julio.

Comments are closed.