The House of Favourite Newspapers

Wabunge Yanga SC waanza na Manji

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji.

WAJUMBE wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga ambao miongoni mwao ni wabunge wenye ushawishi, wanasikia kwa mbaali nyayo za Yusuf Manji akirejea klabuni hapo.

Ingawa wanafanya mambo yao kwa siri sana lakini Championi Jumamosi linajua kwamba wana mikakati mitatu dhidi ya Manji.

 

Kwanza wanamshawishi arejee nafasi ya mwenyekiti, lakini pili ikikwama hiyo atue akiwa muwekezaji na tatu ikishindikana kabisa awe mshauri.

 

Tangu msimu uliopita Yanga imekuwa ikikabiliwa na ukata baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuf Manji kutangaza kujiweka kando kwa madai ya kukabiliwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya kiafya.

 

Hata hivyo, habari kutoka ndani ya Yanga ambazo Championi Jumamosi limezipata zimedai kuwa uongozi wa timu hiyo hivi sasa upo katika mchakato wa kuhakikisha unamrudisha Manji klabuni hapo.

Inadaiwa kuwa baada ya hivi karibuni uongozi wa Yanga kutangaza wajumbe wapya watakaosimamia ucha¬guzi wao ambao baadhi yao ni Wabunge, harakati za kuhakikisha Manji anarejea klabuni kwa njia yoyote ile kabla ya uchaguzi huo kufanyika kwa mara nyingine zimeanza kwa kishindo.

 

“Mchakato kwa ajili ya kupata viongozi wapya unaendelea vizuri lakini pia tunaendelea na mipango mingine ya kuhakikisha tunaimarisha uchumi wa klabu yetu.

 

“Tumeshafanya mazungumzo na wadau mbalimbali akiwemo Manji kwa ajili ya kuona ni jinsi gani timu yetu inarudi katika hali yake ya zamani.

 

“Kwa hiyo kama mipango yetu hiyo itakaa sawa, basi mambo yatakuwa sawa. Tumuombe Mungu tu atuwezeshe kila kitu kiende kama tulivyopanga,” kilisema chanzo makini na cha kuaminika.

 

Hata hivyo, alipoulizwa na Championi Jumamosi kuhusiana na hilo, Mwenyekiti mpya Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Venance Mwamoto alisema kuwa: “Kwa sasa sipo tayari kusema chochote kuhusiana na hilo, kwa sababu bado hatujaanza kazi rasmi tangu tulipoteuliwa kwa ajili ya zoezi hilo la uchaguzi.

 

“Hata hivyo, siku ya Machi 5, ambayo itakuwa siku ya Jumanne tutakutana na uon¬gozi kwa ajili ya kujua kama tutaanza upya mchakato huo wa uchaguzi au tutaendelea ulipoishia ule wa kwanza.
“Kwa hiyo baada hapo ndipo nitakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia suala zima la Manji.”

Stori: Sweetbert Lukonge na Musa Mateja

Comments are closed.