Simba Yapiga Mtu Saba Dar

KWENYE Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite kuna mbwembwe kwelikweli. Unaambiwa jana Simba Queens imempiga mtu 7-0. Ni  wale Evergreen Queens. Matokeo hayo yameipandisha Simba hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ambayo Bia ya Serengeti Lite imepania kuikuza kwelikweli.

 

Huo ni ushindi wa pili wa Simba kwenye mzunguko wa pili wa ligi hiyo, kwani mechi ya kwanza waliifunga Tanzanite kwa mabao 4-0.

 

Mabao ya Simba yalifungwa na Amina Ramadhani, alifunga `hat-trick’, Mwanahamisi Omary akifunga moja, Mrundi Joelle Bukuru alifunga mawili na Opah Clement akifunga moja.

Akizungumza na Spoti Xtra baada ya mchezo huo, Kocha wa Simba Queens, Mussa Mgosi alisema umekuwa ushindi muhimu kwao kwa kuwa umewasaidia kupanda hadi nafasi ya pili, wakiwa na pointi 28, nyuma ya JKT Queen’s wenye 36.

 

“Umekuwa ni ushindi mzuri sana kwetu kwa kuwa umetufanya tupande hadi nafasi ya pili kwenye msimamo, ubora wa kikosi chetu ni kitu kingine ambacho kimetupa matokeo hayo,” alisema Mgosi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba ya wakubwa.

 

 

Toa comment