The House of Favourite Newspapers

Championi: Tuna imani na Taifa Stars, fanyeni kweli

 

GAZETI la Championi kwa niamba ya makampuni yote ya Global Group tunaamini timu ya taifa ya Tanzania itatuwakilisha vema katika mchezo wa keshokutwa Jumapili dhidi ya Uganda na kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (2019).

 

Wachezaji na benchi la ufundi wanatakiwa kutambua kuwa mamilioni ya Watanzania wapo nyuma yao, ushindi wa Jumapili kama ukituwezesha kufuzu, basi watambue kuwa historia mpya itakuwa ikiandikwa na kuna vizazi vingi ambavyo vitakuja kukumbuka hicho kitakachotokea.

Tangu Tanzania ilipofuzu kucheza michuano hiyo mwaka 1980, kuna vizazi vingi hapo kati vimepita na kusoma tu kwenye historia kuwa Tanzania iliwahi kushinda, hivyo, hii ni nafasi ya kipekee na inawezekana ikawa ngumu kujirudia.

 

Muhimu wadau wengi tujitokeze kwa wingi uwanjani kuwashangilia mashujaa wetu. Go Taifa Stars Go!

Comments are closed.