The House of Favourite Newspapers

Zahera ataja mechi moja ya ubingwa

Kocha wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera.

 

JUMATATU ijayo Yanga watakuwa na kibarua kizito cha kupambania pointi tatu na Azam FC, sasa Kocha wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera amesema akiwatandika wapinzani wake hao basi watakuwa na asilimia kubwa ya kuchukua ubingwa wa ligi.

 

Yanga wenye pointi 74, wakiwa ndiyo vinara wa ligi, watapambana na Azam FC wanaoshika nafasi ya pili katika mechi ambayo itakuwa ngumu kwa pande zote mbili itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Kocha huyu ambaye ni msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo, ameliambia Championi Jumatano, kuwa mechi hiyo kwa sasa ndiyo ngumu kwao na wamekuwa wakitafuta mbinu za kupata ushindi.

 

“Hii ni mechi ngumu kwetu, hawa Azam ni timu nzuri na wenye ushindani wa hali ya juu. Tunawatafutia namna bora ya kupata ushindi mbele yao, tunaamini tukishinda tutajiweka katika mazingira mazuri zaidi ya kuchukua ubingwa.

 

“Kama tukishinda mbele yao, ina maana itakuwa sasa tufungwe mechi nne, ndiyo wao tena watupate, kitu kikubwa kwa sasa tunapanga mbinu ambazo zitatupa pointi mbele yao ili tuwe na nafasi ya ubingwa,” alisema Zahera.

Comments are closed.