The House of Favourite Newspapers

Simba Yawatandika Alliance 2-0, Niyonzima Atupia

Kikosi cha timu ya Simba.

SIMBA jana Jumanne walishusha hasira zao kwa Alliance Schools, baada ya kuwatandika mabao 2-0 ikiwa ni siku chache baada ya kufungwa na Kagera Sugar. Simba waliingia kwenye mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mabao 2-1 na Kagera Sugar kwenye mechi yao ya mwisho ya ligi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

 

Simba wanaofundishwa na Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems, walipata ushindi huo muhimu na kuwafanya warudi kwenye mstari wa kuwania ubingwa wakiwa na vita na wapinzani wao Yanga ambao wapo kileleni mwa msimamo.

Simba walipata mabao yao katika kila kipindi, ambapo kiungo Haruna Niyonzima ndiye aliyekuwa wa kwanza kufunga baada ya kufunga bao safi la kideo kabla ya Emmanuel Okwi aliyetokea benchi kufunga bao la pili. Huu ni ushindi wa 20, Simba wanaupata msimu huu baada ya kucheza mechi 25.

 

Wamefungwa mbili na sare tatu Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 63, ikiwa ni pointi 11 nyuma ya Yanga wenye pointi 74. Baada ya kuifunga Alliance kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, kesho Alhamisi, Simba itacheza dhidi ya KMC uwanjani hapo katika mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu Bara

Comments are closed.