The House of Favourite Newspapers

WAKATI MOND AKISUASUA KWA TANASHA… GUMZO NDOA YA ZARI!

UKISIKIA kupindua meza kibabe ndiyo huku anakotaka kufanya mrembo kutoka Uganda Zarinah Hassan ‘Zari’, shemeji wa zamani wa Wabongo kwa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’.

 

VYANZO VYADOKEZA

Ijumaa Wikienda limedokezwa na vyanzo vyake kuwa, Zari yuko mbioni kufunga ndoa na mpenzi wake mpya aliyemtambulisha kwa jina la Mr M ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akimsifu kwenye mitandao ya kijamii mpaka basi.

Ikumbukwe kwamba, tangu mrembo huyo aamue kutafuta mrithi wa penzi la Diamond na kumwanika wazi gumzo limekuwa kubwa mitandaoni kuhusu uhusiano wao na sasa taarifa za kunukia kwa ndoa yao imechochea zaidi minong’ono.

 

VUTA KUMBUKUMBU

Mwishoni mwa mwaka 2014, penzi la Diamond na Zari lilichipuka kwa kasi na kuleta faida ya watoto wawili; Tiffah na Nillan.

Wakati watoto hao wakizaliwa mpaka penzi lao linavunjia rasmi, Diamond hakuwa amemuoa Zari, licha ya mara kadhaa kuahidi kufunga ndoa na mrembo huyo.

Mwisho wa picha la uhusiano wao ni kila mmoja kuanza maisha yake na kuanzisha uhusiano mpya ambapo Diamond alijisogeza kwa msichana Tanasha Donna kutoka Kenya na Zari kuangukia mikononi mwa Mr M, raia wa Afrika Kusini ambaye anatajwa kuwa na mkwanja wa kufa mtu.

 

NDOA YA ZARI YANUKIA

Unaweza kusema ni kama mtu ambaye hataki kuushabikia kabisa wimbo wa MwanaFA wa “Utaoa lini?” Na jibu kuwa “Bado Niponipo Kwanza,” Mr M anatajwa na vyanzo vyetu kuwa ameamua kuingia mazima kwa Zari na kwamba siku chache zijazo amejipanga kumposa na kumuoa.

“Hawako kwenye penzi la maigizo, wamekusudia kuoana kabisa, mwanaume ameamua wahalalishe penzi lao kidini,” Chanzo kilicho karibu na Zari kililiambia Ijumaa Wikienda kwa siri.

ZARI CHEKO KAMA LOTE

Ukisoma posti ya Zari aliyoiweka kwenye Instagram yake hivi karibuni huwezi kusubiri mwingine akuambie Mganda huyo anauchekeleaje kweli uhusiano wake huo mpya.

Kwa ushahidi mdogo hebu soma posti yake hii kwa Kimombo halafu chini utatafuniwa kwa Kishwahili lau kujua alichomaanisha kwamba yuko ‘hepi’ na Mr M wake.

“I love you so much Mr M, it’s not the material things you shower me with, I’ve seen those and even bigger and better.

But, its you, your heart, your whole being and how you make me and my kids feel. It takes alot of courage from YOU Mr M..5kids, 38, wow… you Heaven sent babe, That said, I end here! I l you

 

Ilisomeka hivyo posti aliyoiambatanisha na picha akiwa amekumbatatiwa na mwanaume huyo ambaye haonekani usoni ambapo kwa Kiswahili alimaanisha hivi: “Nakupenda sana Mr M, si kwa vitu unavyonipa kwa wingi pekee, nimeshaviona vingi, tena vikubwa! Lakini ni kwa ajili yako, moyo wako, jinsi ulivyo na jinsi unavyonifanya mimi na watoto wangu tujisikie vizuri. Inahitaji ujasiri sana kwako Mr M, watoto watano na miaka yangu 38, wow…. Umetumwa kutoka mbinguni mpenzi, naishia hapa!. Nakupenda.

 

WAPAMBE WAKE SASA

Baada ya posti hiyo, wapambe wa mambo ya watu walianza kujitokeza kuandika watakacho ambapo wengi walionesha kumtakia heri Zari katika uhusiano huo mpya.

Mmoja aliandika hivi: “Kesho tutakuwa na kikao cha dharura kuvunja rasmi kamati ya watembea kwa magoti toka Dar mpaka South.”

 

Mwingine: “Olewa zako mrembo wangu, shemeji yangu wa zamani, alishindwa kukutunza, wenye meno wamekuchukua.”

Kufanya mambo yasiwe mengi hizo ni baadhi ya posti zilizozua gumzo la aina yake mitandaoni kuonesha kwamba Zari bado anajadiliwa na Wabongo licha ya kumwagana na Diamond.

 

SHEREHE KUTIKISA

Chanzo chetu kinasema kuwa ingawa bado mipango ya harusi haijaanza kufanywa rasmi lakini Mr M na Zari wamekusudia kufanya sherehe kubwa ya kifahari ambayo itatikisa siyo Afrika Mashariki tu bali Afrika nzima.

“Bahati nzuri yule mwanaume ana fedha (hakujata anazipata kwa kazi gani?) na Zari kama anavyofahamika; wewe unadhani wanaweza kufanya sherehe ya kitoto?” Chanzo kilihoji kuonesha kwamba itakuwa na kishindo kikubwa.

WATOTO WA DIAMOND

Mara kadhaa katika posti zake Zari amekuwa akimsifu mpenzi wake mpya kwamba ni mwanaume ambaye ana mapenzi ya dhati kwa watoto ambao amemkuta nao wakiwemo wa Diamond.

Hili linaonesha kwamba mwanamke huyo hana wasiwasi juu ya malezi ya watoto wake watano ambao amekuwa akiishi nao baada ya watatu kufiwa na baba yao na wengine kuwa mbali na mzazi wao wa kiume ambaye ni Diamond.

 

DIAMOND NA AHADI ZA NDOA

Kumbukumbu zinaonesha kuwa Diamond amekuwa fundi wa kuahidi kufunga ndoa na wasichana ‘anaodeti’ nao lakini mwisho wa siku huishia kuwamwaga.

Amewahi kumuahidi ndoa Penniel Mungilwa ‘Penny’, Wema Sepetu lakini hakufanya hivyo na sasa ameahidi kumuoa Tanasha lakini bado anasuasua jambo ambalo wengi wanahisi huenda yatamtokea ya Zari na wenzake.

Stori: Mwaandishi Wetu, Ijumaa Wikienda

Comments are closed.