The House of Favourite Newspapers

Zahera ataka rekodi ya dakika 360 Yanga

Mwinyi Zahera.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amefunguka kuwa anataka kumaliza ligi kwa kuhakikisha anashinda mechi zake nne za mwisho ambazo ni sawa na dakika 360, licha ya kuwa na nafasi finyu ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.

 

Zahera anataka rekodi hiyo ikiwa Yanga inaendelea kuongoza ligi kwa pointi 80 wakati Simba ikiwa na pointi 72 katika nafasi ya pili kabla ya mchezo wake wa jana dhidi ya Mbeya City.

 

Yanga imebakiza michezo dhidi ya Biashara United, Ruvu Shooting, Mbeya City na Azam tofauti na Simba wenye mechi tisa.

 

Akizungumza na Championi Juma­mosi, Zahera alisema kuwa lengo lake kwa sasa ni kuona wanamaliza ligi wak­iwa wanashinda mechi hizo ili kujiweka katika nafasi nzuri licha ya nafasi yao ya kutwaa ubingwa kuwa ndogo.

 

“Tumemaliza na ushindi hilo tulitara­jia mapema kulingana na timu ambayo tumecheza nayo, ingawa wachezaji wangu hawakufuata kile ambacho nili­waagiza na kwa sasa tunaangalia katika mechi zilizopo mbele yetu.

 

“Mechi zetu za mwisho ni muhimu kwetu kuweza kupata matokeo na ndiyo jambo la msingi ili tuweze ku­maliza katika nafasi nzuri kwa sababu ukiangalia wenzetu, bado wana mechi nyingi zaidi yetu, hivyo hatuwezi kuwa na uhakika na ubingwa kwa sasa lakini tunahitaji kushinda hizi mechi zilizobaki ili kulinda rekodi yetu,” alisema Zahera.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Comments are closed.