The House of Favourite Newspapers

Breaking: Mjumbe Wa Kamati Ya Utendaji Yanga Afariki

Klabu ya Yanga imepata pigo kufuatia kifo cha mjumbe wake wa kamati ya Utendaji Felix Kibodya.
Kibodya amefariki usiku wa kuamkia leo Ijumaa hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amethibitisha taarifa hizo za kifo cha Kibodya.

 

Mwakalebela amesema Yanga imepata pigo kutokana na msiba huo kwani walikuwa wanategemea nguvu kubwa kutoka kwa marehemu juu ya taaluma yake ya sheria.

Mwakalebela ameongeza kuwa kwasasa klabu yao inafuatilia msiba huo kwa karibu kujua utaratibu wa kamili na kwamba baada ya hapo wataujulisha uma.

Aidha Mwakalebela amesema kuwa uongozi wao ulikuwa na taarifa za kuugua kwake ambapo alianza kupata matatizo ya afya siku chache baada ya kuteuliwa.

Comments are closed.