The House of Favourite Newspapers

MATATIZO YA KINAMAMA WAJAWAZITO SASA BAAAS

Waziri Ummy akisoma risala leo katikamatembezi ya hisani chini ya mpango wa ‘Stand Up for African Mothers’ maarufu kama SU4AM ambayo ni kampeni ya Amref Health Africa

Shirika la kimataifa la Amref Health Africa kwa kushirikiana na Benki ya Azania (ABL) leo waliandaa matembezi ya hisani chini ya mpango wa ‘Stand Up for African Mothers’ maarufu kama SU4AM ambayo ni kampeni ya Amref Health Africa yenye lengo la kuhamasisha watu duniani kote kuhakikisha kuwa kinamama wanapata huduma za msingi wanazohitaji wakati wa ujauzito mpaka kipindi cha kujifungua.

Waziri akimtunukia cheti cha heshima Mkurugenzi wa Mtendaji wa Benki ya Azania (ABL) Charles Itembe, kwa kufanikisha shughuli hiyo.

Katika matembezi hayo yaliyoishia Uwanja wa Green maarufu Uwanja wa Farasi, Oysterbay, Dar, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.

Sehemu ya wageni waalikwa baada ya kumaliza matembezi hayo.

Katika hotuba yake, Waziri Ummy alisema wizara yake ina mipango kabambe ya kuhakikisha wanaboresha sekta ya afya upande wa wakunga ikiwemo kuwaajiri wakutosha ili kuweza kuondokana na tatizo la uhaba wa wakunga. Matembezi hayo yamefanikishwa na taasisi mbalimbali ikiwemo Benki ya Azania na nyinginezo.

Wadau wakimkabidhi Waziri Ummy zawadi maalum ya kumpelekea Makamu wa Rais, Mama Samia ambaye alitarajiwa kuwa mgeni.
Wafanyakazi wa Benki ya Azania wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni wa heshima.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

Comments are closed.