visa

SIMBA YAMPELEKA MO KWA WAZIRI MKUU

Mohamed Ibrahim ‘Mo’

KIUNGO wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Mo’ ametolewa kwa mkopo rasmi na klabu yake kwenda kujiunga na Namungo FC ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu. Mo amejiunga na klabu ya Namungo FC ambayo mlezi wake ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na imepanda ligi kuu.

 

Mchezaji huyo ambaye alikuwa anahusishwa kwenda kwa mkopo KMC, ni moja kati ya wachezaji wa simba ambao msimu uliopita walishindwa kutamba ndani ya kikosi hicho.

 

Akizungumza na spoti Xtra, Meneja wa  nyota huyo, Jamal Kisongo alisema; “Msimu ujao Mo hatakuwa sehemu ya kikosi cha simba atakuwa  katika kikosi cha Namungo FC ambako ametua kwa mkopo na atacheza hapo kwa msimu huo mpya.

 

“Yalikuwa makubaliano yetu na simba ndiyo maana hata kwenye majina ambayo wamepeleka Caf  hakuna jina lake anaenda timu nzuri kikubwa ni yeye kupambana.”

FAINALI YA MISS KINONDONI KUTIKISA DAR JUMAMOSI HII…!
Toa comment