The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Polisi 54 Wamefukuzwa Kazi Kujihusisha na Uhalifu

 

Inspekta Jenerali wa Polisi nchini (IGP), Simon Sirro.

ASKARI 54 wa Jeshi la Polisi nchini wamefukuzwa kazi kati ya Januari hadi Juni mwaka huu (2019) baada ya kubainika kwenda kinyume na maadili ya kazi ikiwamo kufanya vitendo vya uhalifu na kushirikiana na wahalifu.

 

Hayo yamesemwa leo na Inspekta Jenerali wa Polisi nchini (IGP), Simon Sirro wakati wa uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari yaliyopo eneo la Magogo mkoani Geita ambapo amebainisha kwamba miongoni mwa askari hao wamo maofisa, wakaguzi na askari wa kawaida waliokutwa na makosa mbalimbali.

 

Uzinduzi huo ulifanywa na Rais John Magufuli ambaye yuko katika ziara ya kukagua aendeleo mkoani Geita na Mwanza.

Comments are closed.