The House of Favourite Newspapers

Yanga yatangaza kamati mpya ya mashindano

Kocha Mkuu Mkongomani, Mwinyi Zahera (kulia) akiongea jambo na Kocha Msadizi Noel Mwandila.

UONGOZI mpya wa Yanga chini ya mwenyekiti wake, Dk Mshindo Msolla, jana ulitangaza kamati mpya ya mashindano kwa ajili ya msimu ujao.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache uongozi wa timu hiyo kuzitenganisha kamati mbili zilizokuwa zinafanya kazi pamoja ya usajili na mashindano iliyokuwa chini ya mwenyekiti wake, Frank Kamugisha.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano na kuthibitishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten, kamati hiyo imeanza kazi yake rasmi jana mara baada ya kuteuliwa ambapo itafanya kazi pamoja na Kocha Mkuu Mkongomani, Mwinyi Zahera.

A

Ten aliwataja viongozi wa kamati hiyo mpya ambayo itaongozwa na mwenyekiti wake, Rodgers Gambo na makamu wake, Saad Khimji, huku katibu akiwa Edwin Mshagama.

 

Wajumbe ni Hamad Islam, Yanga Makaga, Ally Kamtande, Leonard Bugomola, Said Side, Bunnah Kamoli, Soud Mlinda, Tom Lukuvi, Martin Mwampashi, Hamza Jabir, Edward Urio, Kawina Konde na Abednego Ainea.

 

“Hiyo ndiyo kamati yetu mpya ya mashindano ambayo tayari imeanza kufanya kazi rasmi leo (jana), itakutana na benchi la ufundi katika ufanyaji kazi wake,” alisema Ten

Comments are closed.