The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Aahirisha Bunge

0

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameahirisha vikao vya Bunge hadi Machi 30, 2021, na kusema kuwa serikali ipo kwenye utekelezaji wa kujenga shule mpya 1026, kwa kutumia mkopo wa Benki ya Dunia ili kusaidia elimu ya Tanzania na kupunguza uhaba wa shule na madarasa nchini.

Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa amesema kuwa hadi kufikia Desemba mwaka jana Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini (REA) awamu ya tatu ulikuwa umefikia zaidi ya vijiji 10,000 kati ya vijiji 12,317 vilivyopo kote nchini .

Majaliwa amebainisha hayo leo Februari 13 jijini Dodoma alipokuwa akitoa hotuba ya kuhairisha shughuli za Bunge na kubainisha kuwa ufikaji wa umeme katika vijiji hivyo ni sawa na 83.3%.

Aidha, Majaliwa amebainisha kuwa kwa mwaka huu Serikali imetenga Shilingi bilioni 171.9 ili kukamilisha usambazaji wa umeme katika vijiji vilivyobakia.

 

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, sasa naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu liahirishwe hadi tarehe 30 Machi 2021 siku ya Jumanne saa 3:00 asubuhi katika ukumbi huu hapa jijini Dodoma, amesema Waziri Mkuu.

Leave A Reply