The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Maalim Seif Waagwa Z’bar kwa Simanzi

0

VIONGOZI  mbalimbali nchini Tanzania wakiwemo wastaafu wamejitokeza katika uwanja wa Mnazi Mmoja mjini Unguja kumswalia aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad.

 

 

Mwenyekiti huyo wa chama cha ACT-Wazalendo alifariki dunia jana Jumatano Februari 17, 2021 katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

Maalim Seif, gwiji wa siasa nchini,Autazikwa leo kisiwani Pemba ambapo baadhi ya viongozi waliofika kiwanjani hapo ni Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi na Makamu wake wa Pili, Hemed Suleiman Abdulla.

 

 

Wengine ni marais wastaafu wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Aman Abeid Karume, makamu wa rais mstaafu Zanzibar, Dk Ghalib Bilal na makamu mstaafu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.

Leave A Reply