The House of Favourite Newspapers

Mahujaji Wamiminika Mecca kwa Ajili ya Hijja

0
Maelfu ya Mahujaji wakizunguka Kaaba

BAADA  ya miaka miwili kupita bila mahujaji kuhudhuria ibada ya Hijja, mji mtakatifu wa Mecca uliopo Saudi Arabia umeanza kuonyesha dalili ya kurejea kwenye hali ya kawaida.

 

Tukio linatokea wakati mahujaji takribani milioni 1 wanapoanza kufanya ibada ya hijja tangu kuzuka kwa janga la corona mwaka 2019,  janga lililopelekea mataifa mengi kufunga mipaka yao.

 

Mahujaji wamekusanyika mapema siku ya jana Julai 7, 2022 kwa sala za kwanza ikiwa nguzo muhimu kwenye dini ya kiislamu, ibada hiyo ya hijja kwa mwaka huu inatarajiwa kwenda mpaka tarehe 12 Julai, 2022

 

Mahujaji hutumia siku kadhaa kwenye maeneo takatifu wakati wakitumia mapito yanayoaminika kutumiwa na mtume Muhammad takriban miaka 1,400 iliyopita.

 

Moja kati ya tamaduni muhimu katika Ibada ya hijja huwani kuzunguka Kaaba ambapo ni mahala patakatifu zaidi katika dini ya kiislamu.

 

Hijja ni nguzo muhimu kwa kila muislamu mwenye uwezo wa kifedha na kimwili walao mara moja maishani.

 

Leave A Reply