The House of Favourite Newspapers

Sadio Mane Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Tuzo zilizotolewa na Shirikisho la Mpira Barani Afrika (CAF)

0

 

Sadio Mane baada ya kupokea Tuzo yake ya mchezaji bora wa mwaka

Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Bayern Munich na timu ya Taifa ya Senegal Sadio Mane, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika tuzo za CAF Zilizotolewa Usiku wa Julai 21, 2022,

Sadio Mane amekuwa mchezaji wa 10 kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika zaidi ya mara moja.

 

 

Nahodha huyo wa Senegal alitangazwa kuwa mshindi wa 2022 katika hafla ya utoaji wa tuzo za Shirikisho la Soka Afrika mjini Rabat, Morocco siku ya Alhamisi 21 Julai, 2022.

 

 

 

Mane aliongoza akinzidi mchezaji mwenzake wa zamani wa Liverpool Mo Salah na kipa wa Chelsea Msenegali Edouard Mendy ambapo Salah alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu England msimu uliopita, akishinda Kiatu cha Dhahabu akiwa amefunga mabao 23 na kuwa kinara wa pasi za mabao 13.

 

 

Lakini Mane, ambaye aliondoka Liverpool na kusajiliwa na Bayern mwezi Juni, mara mbili alimshinda Salah katika kiwango cha kimataifa.

 

 

 

Senegal ya Mane iliishinda Misri ya Salah katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Februari na kisha tena katika mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia mwezi Machi.

 

 

 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ndiye kipa wa kwanza kuingia tatu bora katika kura ya Mwanasoka Bora wa Afrika tangu 2014 Vincent Enyeama alipoibuka wa tatu.

 

 

Mane anakuwa mchezaji wa sita kutajwa kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka mara mbili haswa. Wengine ni Salah, Didier Drogba, Roger Milla, Nwankwo Kanu na El Hadji Diouf.

 

 

George Weah na Abedi Pele wote ni washindi mara tatu, huku Samuel Eto’o na Yaya Toure wakishinda tuzo hiyo mara nne kila mmoja.

Leave A Reply