The House of Favourite Newspapers

Aliou Cisse, Kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal ashinda Tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka

0
Aliou Cisse, kocha bora wa mwaka 2022-tuzo za CAF

ALIOU Cisse, amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

 

Aliou Cisse, 46, aliiongoza Senegal kushinda kombe lao la kwanza la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon, mapema mwaka huu, baada ya kuishinda Misri kwa mikwaju ya penalti.

 

Pia ameiongoza Simba ya Teranga kufuzu kwa kombe la dunia nchini Qatar baadaye mwaka huu mbele ya Misri katika mechi ya mchujo.

 

Mvulana huyo wa zamani mwenye uwezo mkubwa wa kuinoa timu amekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa tangu 2015 na aliiongoza kutinga fainali ya AFCON mwaka 2019 kabla ya ushindi wao mwaka huu.

 

Aliiongoza Senegal kama nahodha I kwenye kombe la dunia la 2002 huko Japan, ambapo Senegal ilifika robo fainali ya kihistoria, bora zaidi kuliko taifa lolote la Afrika kuwahi kufika kwenye michuano hiyo.

 

Leave A Reply