The House of Favourite Newspapers

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kinara Maadhimisho Wiki ya Chakula

0

 

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umeibuka na kuwa mshindi katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Simiyu.

 

Mbali na ushindi na huo, pia NFRA imepata mafanikio makubwa katika Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambayo imekuwa ni nguzo imara ya kuongeza ufanisi wa NFRA katika utekelezaji wa majukumu yake.

 

Taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, imeleeza kuwa mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuongezeka kwa ununuzi wa Akiba ya chakula ambapo kumekuwa na ongezeko la ununuzi kutoka takriban tani 58,000 kufikia zaidi ya tani 110,000 za nafaka kwa mwaka 2021/2022.

 

Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa akiba ya chakula ambalo limewezesha wakala kuwa na akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya kuhudumia kwa wakati mahitaji mbalimbali ya dharura au upungufu wa chakula unaoweza kujitokeza nchini.

 

Kupunguza kasi ya mfumuko wa bei za nafaka ni mafanikio mengine ambapo wakala umefanikiwa kukabiliana na makali ya mfumuko wa bei za nafaka katika maeneo yaliyohudumiwa, kwa lengo la kupunguza makali kwa kuongeza upatikanaji wa nafaka katika masoko hivyo kuleta unafuu katika maisha ya wananchi.

 

 

Kwa kuanzia, Wakala unahudumia Halmashauri za Bunda, Sengerema, Geita, Nzega, Liwale, Nachingwea, Longido, Loliondo na Monduli ambapo takriban tani 3,000 zimepelekwa katika maeneo hayo. Wakala kwa niaba ya Serikali umejipanga kuhudumia halmashauri nyingine zinazoweza kuthibitika kuwa na upungufu wa chakula ili kuleta unafuu kwa wananchi.

 

Mafanikio mengine ni pamoj ana kukamilisha sehemu ya mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka, kuwa na soko la uhakika la wakulima, kuchangia mapato ya Halmashauri na Serikali Kuu na kutoa ajira kwa wananchi na Sekta Binafsi pamoja na kutoa elimu kwa wadau kupitia matukio mbalimbali: Wakala umekuwa ukitoa elimu katika masuala ya uhifadhi kwa Wananchi mbalimbali kupitia njia mbalimbali ikiwamo vyombo vya habari na matukio ya Kitaifa na Kimataifa

Leave A Reply