The House of Favourite Newspapers

Mzungu Singida Aipa Ubingwa Yanga Ligi Kuu Bara Msimu Huu

0
Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Mholanzi, Hans Van Pluijm.

KASI ya kikosi cha Yanga katika vita ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu imemshtua Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Mholanzi, Hans Van Pluijm ambaye ameweka wazi kwamba timu hiyo inastahili kuwa kwenye nafasi ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Alhamisi ya wiki hii, Pluijm alishuhudia kikosi chake cha Singida Big Stars kikipokea kichapo cha mabao 0-2 nyumbani kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida dhidi ya Yanga, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Ushindi huo uliifanya Yanga kuzidi kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao baada ya kufikisha pointi 71, ambapo sasa wanahitaji pointi tatu tu kutangazwa mabingwa katika mechi tatu zilizosalia.

Akizungumza na Spoti Xtra, Pluijm alisema: “Ulikuwa mchezo mzuri na wa ushindani mkubwa kwa pande zote mbili, tulifanya makosa wakayatumia na kupata ushindi, tumekaa na wachezaji wetu na kuelekezana kipi tunapaswa kurekebisha kuelekea michezo ijayo.

“Yanga ni timu bora sana na sio kwa bahati mbaya wapo kwenye nafasi ya kushinda ubingwa, nadhani wanastahili kuwa walipo kutokana na ubora wa kikosi walichonacho.”

STORI NA JOEL THOMAS

MISS BELLA ATOBOA SIRI KUFUNGA NDOA YA JADI-“WALIOLETA DINI WAMELETA MAPENZI JINSIA MOJA”

Leave A Reply