The House of Favourite Newspapers

Simba Yaishushia Azam Mziki Kamili Leo Jumapili Kwenye Mchezo wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation

0

BENCHI la Ufundi la Simba, chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ limebainisha kuwa, mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Azam FC watacheza wachezaji wote kwa kuwa wanatambua wajibu ni lazima utimizwe.

Leo Jumapili, Simba inatarajiwa kumenyana na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation, Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Namungo, Simba ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na mtupiaji alikuwa Jean Baleke ambaye anafikisha bao lake la 8 kwenye ligi.

Katika mazoezi ya mwisho, miongoni mwa wachezaji wa Simba waliofanya mazoezi ni Clatous Chama, Saidi Ntibanzokiza, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe, Joash Onyango na Pape Sakho.

Juma Mgunda, Kocha Msaidizi wa Simba, alisema kuwa ratiba ilikuwa wazi kwa kila mchezaji kuhusu mchezo wao dhidi ya Azam FC, hivyo wote wapo tayari kucheza.

“Ni mchezo ambao upo kwenye ratiba na wachezaji wanatambua umuhimu wa kupata ushindi kwenye mchezo huo, hivyo maandalizi kuhusu mchezo huo yote yamekamilika na mchezaji atakayepangwa anajua atavaa gwanda kuipambania timu.

“Wale wote ambao wamesajiliwa ndani ya Simba ni lazima wacheze na watimize wajibu wao, wapinzani tunawaheshimu kwani sio timu mbaya, kufika hatua hii ya nusu fainali tunaamini itakuwa kazi kubwa,” alisema Mgunda.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA

MISS BELLA ATOBOA SIRI KUFUNGA NDOA YA JADI-“WALIOLETA DINI WAMELETA MAPENZI JINSIA MOJA”

Leave A Reply