The House of Favourite Newspapers

Zaidi Ya Vijana 2500 Kukutanishwa Na UVCCM Ulanga Moro

0
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ulanga, Shahista Suleman.

Morogoro, 6 Juni 2023:Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Ulanga unatarajia kufanya tamasha la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwakutanisha vijana zaidi ya elfu mbili mia tano waliopo wilaya ya Ulanga kupongeza Rais Samia kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kuinua vijana kiuchumi kupitia ajira na utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ulanga, Shahista Suleman amesema tamasha hilo linatarajia kufanyika Juni 10 mwaka huu ikiwa ni katika kumtia moyo Rais Samia kutokana na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo hasa katika sekta ya afya, maji, elimu na ajira kwa vijana

Mkutano huo ukiendelea.

Naye Katibu wa Hamasa na Chipukizi wilaya hiyo, Thomas Machupa amebainisha kuwa pamoja na mambo mengine wanashukuru kwa serikali na mbunge wa jimbo hilo kuwawezesha vijana katika vikundi 7 ambavyo vilipatiwa Pampu za kilimo cha umwagiliaji pamoja na mkopo wa pikipiki 65 kwaajili ya vijana wa bodaboda ndani ya mwaka mmoja tangu viongozi wapya wa UVCCM wilaya hiyo kuingia madarakani. HABARI/PICHA ZOTE NA MWAJUMA RAMBO /GPL Morogoro

Leave A Reply