The House of Favourite Newspapers

Global Education Link Yahitimisha Maonesho Ya Vyuo Vikuu Kwa Mafaniko Makubwa

0
Wananchi wakihudumiwa kwenye banda la Global Education Link.

Dar es Salaam 22 Julai 2023: Taasisi ya uwakala wa vyuo vikuu vya nje ya nchi Global Education Link imehitimisha maonesho ya vyuo vikuu kwa mafaniko makubwa huku wanafunzi wengi wakijisajili.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu nje ya nchi Global Education Link, Abdulmalik Mollel amesema lengo kubwa ni kuhakikisha wanatoa changamoto ya wanafunzi ambao wanatoka Tanzania kwenda kwenye vyuo vikuu vya nje ya nchi.

Baadhi ya wanafunzi waliotembelea katika Banda la Global Education Link wakipata maelekezo katika Banda hilo.

Amesema kwa ujumla vyuo vikuu wanavyodili navyo kwenye maonesho hayo ni pamoja na vyuo vikuu vya UK, Canada, India, Australia, Syprus, Mauritius, Uturuki, Malaysia na nchi nyingine mbalimbali.

“Maonesho haya yamefana  sana kwa sababu tumekuwa tukipokea wanafunzi wanaohitaji kwenda kusoma nje ya nchi imekuwa ni kubwa na pia vyuo vikuu vya Tanzania vilivyopo humu vimekutana na kushikiana na vyuo vikuu vya nje ya nchi ili kubadilishana uzoefu ili kuhakikisha tunamboresha Mtanzania kwa njia yoyote katika kupitia mifumo ya ufundishaji katika elimu ya juu.

“Kwa hiyo vyuo vikuu vya nje tukiunganisha na vyuo vikuu vya kwetu, hawa wakifanya kazi kwa pamoja maana yake tuna uhakikia kabisa yale tunayoyaona kwao kama maendeleo, basi na sisi tunayahitaji kuwa hayo kama maendeleo, kama wao wanatengeneza solar sisi tunaagiza Solar basi tunategemea watengenezaji solar kwa kupitia vyuo vyetu vikuu, vinaweza vikatengeneza Solar kupitia vyuo vikuu vyetu hatuna tatizo la kitaaluma wala kiakili inawezekana tuna changamoto ndogo ya kiteknolojia kwa hiyo sasa kwa  kutumia mifumo hii ya muungano tatizo hilo ndipo linaondoka.

Pia ameishukuru serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuandaa maonesho hayo kwa kupitia tume ya vyuo vikuu Tanzania TCU na hitimisho lake ni Leo Julai 22,2023.

Leave A Reply