The House of Favourite Newspapers

Kenya: Nyumba Ya Mtoto Wa Uhuru Kenyatta Yadaiwa Kuvamiwa Na Polisi

0
Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta

Kikosi cha maafisa wa polisi kimemvamia makazi ya Mtoto wa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta huko Karen.

Akizungumza huko Karen, Uhuru alithibitisha kuwa polisi walivamia nyumba ya Mtoto wake wa mwisho Jomo Kenyatta, wakitafuta bunduki na silaha zingine.

Uhuru amedai kuwa maafisa wanaoripotiwa kutoka kwa Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai walikuwa wakitumia magari yenye nambari za Usajili za Sudan.

“Nilipata ripoti kutoka kwa mwanangu kwamba kulikuwa na watu nyumbani wanaodai kuwa maafisa wa DCI kwenye gari lililokuwa na usajili wa Sudan na kudai kuwa walitaka kumuona na kuzungumza naye,”

Uhuru amesema ikiwa utawala wa Kenya Kwanza unamlenga, basi wanapaswa kumfuata kama mtu binafsi.

Uhuru ameongeza kuwa kukaa Kwake kimya baada ya Ruto mamlaka hakumaanishi kuwa anaogopa chochote. “Mwanangu amevamiwa nyumbani na sasa najiuliza hii serikali inataka nini?

Kama ni mimi wananilenga basi waje tu, kukaa kimya kwangu haimaanishi kuwa naogopa, njoo kwangu. Mamangu ana uhusiano gani na. siasa? Watoto wangu wana uhusiano gani na chochote mnachotafuta?” amesema Uhuru akionyesha kukarishwa na Kitendo hicho.

NONDO ZA SHIGONGO KWENYE KONGAMANO LA UVCCM SENGEREMA WAJIPANGE NA JESHI MITANDAONI!

Leave A Reply