The House of Favourite Newspapers

Benki ya Mwanga Hakika Yaja na “PINK Mwanamke Account” Kuwawezesha Wanawake Kifedha

0
Meneja wa Biashara wa Mwanga Hakika Bank, Judith Halinga akizungumza wakati wa hafla hiyo.

*Wateja kupata uhakika wa kuweka akiba na kufurahia faida kwenye amana zao

Benki ya Mwanga Hakika Limited imekuja na huduma ya Pinki Mwanamke Account ambayo itawawezesha wateja wanawake kuweka akiba huku wakipata faida mbalimbali ikiwamo kupata faida ya kwenye amana zao.

Akaunti hii ni rafiki kwa wanawake wa aina zote na ni mahususi kwa wanawake wenye ndoto za muda mfupi na mrefu ambapo itawawezesha kuyafikia malengo hayo bila kutumia nguvu kubwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja wa Biashara wa Mwanga Hakika Bank, Judith Halinga alisema benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasogeza huduma za kibenki karibu na wateja ili kuboresha Maisha ya watanzania.


“Benki yetu toka ilipopata hadhi ya kuwa benki rasmi ya biashara, tumekuwa mstari wa mbele kuendeleza ajenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kwa kuja na huduma za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya kifedha,” alisema na kuongeza;

“Hii inathibitika leo ambapo tunazindua Pinki Mwanamke Account ambayo itaboresha huduma za kibenki kwenye soko.Kwa kupitia akaunti hii, wanawake nchini bila kujali kipato chao wanapata fursa ya kuhifadhi fedha zao kwa uhakika zaidi huku amana zao zikiwasaidia kupata faida mbali na kutunza fedha,” alisema.
Huduma hii imekuja wakati ambapo watanzania wengi wamekuwa na muamko mkubwa wa kufuatilia matumizi yao ya fedha.

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa Fin Scope ya mwaka 2023 inaonesha asilimia 77 ya watanzania wanafuatilia matumizi ya pesa zao.
Hii ina maana kwamba uelewa juu ya umuhimu wa kuwa na taarifa za mapato na matumizi umeongezeka hivyo ni muhimu kwa taasisi kuja na suluhu za kifedha zitakazowasaidia kufanikisha malengo yao.

Huduma hii inakuja na manufaa mbalimbali kama kufungua akaunti bure, hakuna makato ya mwezi na riba itakokotolewa na kulipwa kila mwezi.
Zaidi ya hilo, akaunti hiyo itawawezesha wateja kupata mikopo bila riba ambayo itawasaidia kufanikisha malengo ya muda mfupi bila kuharibu au kugusa amana zao (savings).
“Kama benki inayokua kwa kasi, tumeenda mbali zaidi na kuja na suluhu ambayo itakidhi mahitaji ya watanzania wengi zaidi.Tunaamini kwamba kupitia akaunti hii watanzania wengi zaidi bila kujali kipato chao watakuwa na uwezo wa kupatan huduma za kibenki na kufungua milango ya mafanikio,” alisema Mkurugenzi Mtendaji Jagjit Singh.

 

Leave A Reply