The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri Wa Afya Zanzibar Atoa Neno Patadawa Ya Tigo Pesa Ikizinduliwa

0
Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (katikati) kwenye uzinduzi huo.

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Afya, imeitaka kampuni ya simu ya mkononi Tigo Zantel na Laina Finance Limited kuangalia uwezekano mwengine wa kurahisha huduma za upatikanaji wa bidhaa mbalimbali kwa wateja wao hasa wakati wa dharura.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Hassan Khamis Hafidh, ameeleza hayo wakati akizindua huduma ya Pata Dawa kupitia simu ya Mkononi Tigo Zantel kwa kushirikiana Laina Finance Limited katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege.

Aidha, ameipongeza Tigo Zantel na Laina Finance kuja na program hiyo ya pata dawa ambayo itamuwezesha mtu na mtumiaji wa mtandao huo kupata huduma za dawa kwa njia ya mkopo na kurudisha fedha hizo kwa kipindi cha siku kumi na kuwatka pia kubuni huduma nyengine mbalimbali ambazo zitaweza kuwasaidia wateja wao hasa katika kipindi cha dharura.

Huduma mpya ya ‘Pata Dawa’ kutoka Tigo Pesa ni fursa mpya kutoka TigoZantel ambayo imehamasishwa na mfumo wa huduma za afya Zanzibar ambao unatoa huduma za matibabu bure kwa wananchi huku ukihitaji wao kujikimu katika kununua dawa zao.

Akizungumza Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha, amesema kwa kutambua jitihada za serikali na uhitaji wa wananchi, Tigo Zantel imeshirikiana na LAINA Finance, kuleta suluhisho ambalo litakidhi mahitaji ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla katika masuala ya matibabu.

“Huduma hii ikiwa ndiyo suluhisho la kwanza la Huduma Halal za fedha kwa njia ya kidijitali kwa utaratibu wa Murabah nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla imeundwa kutoa mpango wa malipo unaofaa zaidi kwa dawa zinazopatikana katika hospitali na maduka ya dawa yaliyoidhinishwa hapa Zanzibar yanayopokea Malipo kupitia Lipa Kwa Simu ya Tigo Pesa,” amesema Angelica.

Leave A Reply