The House of Favourite Newspapers

Chasambi amtaja aliye nyuma ya bao lake Ligi ya Mabingwa Afrika

0
Nyota wa klabu ya Yanga, Ladack Chasambi.

LADACK Chasambi nyota wa Simba ameweka wazi kuwa maelekezo aliyopewa na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha ni sababu yay eye kufunga bao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba iliyopo kundi B kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika inaungana na ASEC Mimosas kutinga hatua ya robo fainali kutoka kwenye kundi hilo ambapo ilikusanya pointi 9 kibindoni baada ya kucheza mechi sita.

Mchezo wa sita ilikuwa Machi 2 2024 dhidi ya Jwaneng Galaxy, ubao ulisoma Simba 6-0 Jwaneng Galaxy, bao la ufunguzi lilifungwa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 7 na Chasambi ambaye ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho alifunga bao lake la kwanza katika Ligi ya Mabingwa Afrika dakika ya 84.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo huo Chasambi aliingia kuchukua nafasi ya Pa Jobe aliyefunga bao moja dakika ya 14 kwenye mchezo huo uliokuwa umeshikilia hatma ya Simba kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chasambi amesema: “Furaha kubwa kuona kwamba tumefanikiwa kufika hatua ya robo fainali na kuhusu kufunga ni sehemu ya furaha kwani maelekezo ambayo nilipewa na mwalimu nilifuata na mwisho tukapata ushindi kwenye mchezo wetu muhimu.

“Kwa mechi zinazofuata tuna amini kwamba tutafanya kazi kubwa kupata matokeo muhimu ni kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kwani kazi bado inaendelea na tutafanya vizuri nina amini hivyo,”.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka

MAKONDA ANAZUNGUMZA JAMBO ZITO MUDA HUU MBELE ya NYOMI LA WAANDISHI WA HABARI…

Leave A Reply